Skip to main content

Jinsi Ya Kulipwa YouTube

Bila shaka umeshasikia sana kuwa watu huingiza fedha kupitia channel zao za Youtube, lakini ni vipi fedha hizo huingia?
buy-adsense-safe-youtube-views
Je wale wenye views nyingi kama Diamond Platnumz ndio hupata fedha nyingi zaidi? Ni views ngapi unazohitaji ile kuingiza fedha kwenye YouTube? Hili ni swali la kawaida ambalo watu huuliza na jibu lake litategemea na nani umemuuliza.
Unaweza kuwa umesikia kuwa utaingiza dola moja kwa kila views 1,000 au $1,000 kwa views milioni moja. Wengine husema ni $5 kwa views 1000.
Mtandao wa videopower.org unadai kuwa tunauliza swali lisilo sahihi na kwamba tunatakiwa kuuliza ‘ni engagement gani inayohitajika ili kuingiza fedha kwenye Youtube?
Mtandao huo unasema huingizi fedha kwa kuzingatia kiasi cha views unachopata. Unatengeneza fedha kwa kuzingatia engagement ya watu kwenye tangazo.
Hapa engagement inamaanisha ni mtu kubofya na kuangalia tangazo kwa zaidi ya sekunde 30. Matangazo ya YouTube yanawezesha kwenye mfumo wa Adwords. Makampuni huchagua kuweka matangazo kwa njia mbili kuu; Cost Per Click (CPC) au Cost Per View (CPV).
Cost Per Click (CPC)
CPC ni pale kampuni inayotangaza inalipa fedha kwa kuzingatia clicks. Kwahiyo kama keyword fulani ikiwa na CPC ya $3 na mtu akaclick tangazo hilo, itaichaji kampuni hiyo $3. Maneno haya ya matangazo hutokea chini ya screen wakati unatazama video na huweza pia kutokea kama banner ya square upande wa kulia wa channel yako.
Cost Per View (CPV)
CPV ni pale kampuni inayotangaza inalipa fedha kwa kulingana na views. View kwa kampuni inayotangaza (advertiser) inamaanisha kuwa mtu anaangalia tangazo kwa walau sekunde 30 au nusu ya tangazo.
Mtu huyo anaweza kuclick tangazo hilo hata mara 50 lakini bado kampuni inayotangaza isitozwe kwasababu hailipi kwa click, wanalipa kwa view.
Kampuni inayotangaza hulipa tu pale mtu anapoclick au kuangalia tangazo kwa sekunde 30. Hii ndio maana huwezi kugeuza views za channel yako kuwa fedha. Kama video yako ikiangaliwa mara milioni 10 lakini hakuna mtu aliyeangalia au kuclick tangazo, huwezi kuingiza fedha yoyote.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kufanya Biashara Mtandaoni. Hizi Hapa Ni Biashara Tano za Kuanza Nazo

Wajasiriamali wengi wamekuwa wakitafuta mbinu mbalimbali za kufanya biashara aidha kwa kuuza huduma au bidhaa. Lakini wachache sana hasa Afrika ambao wanafikiria kufanya biashara katika intaneti. Kuna mbinu nyingi tofauti za kufanya biashara katika intaneti ambazo zinatoa fursa kwa wajasiriamali kujiongezea kipato. Kinachohitajika ni simu au kompyuta yenye kuunganishwa na mtandao wa intaneti na pia kuwa umejiunga na mitandao ya kijamii ,au mmiliki wa tovuti au blogu (ambazo unaweza kupata bure) au barua pepe. Zifuatazo ni baadhi ya programu zinazokuwezesha kupata fedha kupitia intaneti: 1. Kuuza Bidhaa za Biashara Yako Kupitia Tovuti  Unaonesha biadhaa zako na bei,wanunuaji wanaziona na kuweka oda ya manunuzi. Wanalipa kwa Kadi ya Benki Credit /Debit Card) na fedha inaingia katika akaunti yako benki. Au kwa kutumia malipo kwa mfumo wa simu kama M-Pesa ,Tigo Pesa na Airtel Money kwa Tanzania. 2. Kuuza bidhaa za biashara ya watu wengine kupitia tovuti Unajisajili na baad...

Jinsi ya Kutengeneza Channel Youtube.

Karibu tena ndugu msomaji na mtembeleaji wa blog yako pendwa ya Tanzania    ambayo inakupatia elimu itakayokusaidia kucopi na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayotokea kila leo. Katika makala ya leo tutaenda kuzungumzia namna ya kufungua channel ya youtube maarufu kama online TV . Makala hii itakwenda kukupa ujuzi wa namna ambayo utaweza kufungua channel ya youtube wewe mwenyewe, channel ambayo utaweza kuweka video zako na watu wengine wakapata kuziona. MAHITAJI 1 : G mail account 2: Kifaa chako cha kielectoniki (kama computer) 3: Internet connection HATUA ZA KUFUATA 1:Fungua mtandao wa youtube kwenye search engine yako mfano opera mini, mozila firefox. kisha tafuta (search) www.youtube.com kama hivi:- 2:Kisha baada ya hapo itafunguka na utatakiwa kuanza kwa ku  sign in  kama inavyoonekana hapa chini:- 3:Kisha baada ya hapo chagua  g mail  account yako ambayo uta  sign in  nayo ka...

Nufaika na Adsense

Ndio unaweza kupata hela katika blogu yako kwa kutumia programu ya Google Adsense. Google Adsense  ni programu  ambayo inatumiwa na  wamiliki wa blogu na tovuti (Publishers), kuonyesha matangazo ya Google ( Google Adwords ) Unachotakiwa kufanya ni kujisajili katika programu hii Google Adsense, wao wataikagua blogu yako na kama blogu yako au tovuti yako itakizi mahitaji yao basi watakupa kibali na namna ya kuweza wewe kuweka matangazo yao kwako. Matangazo haya  ya Google Adsense yatakupa wewe hela kwa  KUBOFWA  (Clicks) na  KUONEKANA  (Impressions). Angalizo Hutakiwi Kubofya (Click) matangazo haya wewe mwenyewe. Acha watu wanaotembelea blogu au tovuti yako wabofye wao kwa mahitaji yao. Google Adsense wanayo namna ya kuangalia kama unafanya mchezo wa kubofya matangazo wewe mwenyewe na wakigundua hili hakuna onyo wanakufungia huduma hiyo. Sasa ili uweze kupata Bofya (clicks) za kutosha pamoja na muonekano (Impressions) lazima blogu au Tov...