Bila shaka umeshasikia sana kuwa watu huingiza fedha kupitia channel zao za Youtube, lakini ni vipi fedha hizo huingia?

Je wale wenye views nyingi kama Diamond Platnumz ndio hupata fedha nyingi zaidi? Ni views ngapi unazohitaji ile kuingiza fedha kwenye YouTube? Hili ni swali la kawaida ambalo watu huuliza na jibu lake litategemea na nani umemuuliza.
Unaweza kuwa umesikia kuwa utaingiza dola moja kwa kila views 1,000 au $1,000 kwa views milioni moja. Wengine husema ni $5 kwa views 1000.
Mtandao wa videopower.org unadai kuwa tunauliza swali lisilo sahihi na kwamba tunatakiwa kuuliza ‘ni engagement gani inayohitajika ili kuingiza fedha kwenye Youtube?
Mtandao huo unasema huingizi fedha kwa kuzingatia kiasi cha views unachopata. Unatengeneza fedha kwa kuzingatia engagement ya watu kwenye tangazo.
Hapa engagement inamaanisha ni mtu kubofya na kuangalia tangazo kwa zaidi ya sekunde 30. Matangazo ya YouTube yanawezesha kwenye mfumo wa Adwords. Makampuni huchagua kuweka matangazo kwa njia mbili kuu; Cost Per Click (CPC) au Cost Per View (CPV).
Cost Per Click (CPC)
CPC ni pale kampuni inayotangaza inalipa fedha kwa kuzingatia clicks. Kwahiyo kama keyword fulani ikiwa na CPC ya $3 na mtu akaclick tangazo hilo, itaichaji kampuni hiyo $3. Maneno haya ya matangazo hutokea chini ya screen wakati unatazama video na huweza pia kutokea kama banner ya square upande wa kulia wa channel yako.
Cost Per View (CPV)
CPV ni pale kampuni inayotangaza inalipa fedha kwa kulingana na views. View kwa kampuni inayotangaza (advertiser) inamaanisha kuwa mtu anaangalia tangazo kwa walau sekunde 30 au nusu ya tangazo.
Mtu huyo anaweza kuclick tangazo hilo hata mara 50 lakini bado kampuni inayotangaza isitozwe kwasababu hailipi kwa click, wanalipa kwa view.
Kampuni inayotangaza hulipa tu pale mtu anapoclick au kuangalia tangazo kwa sekunde 30. Hii ndio maana huwezi kugeuza views za channel yako kuwa fedha. Kama video yako ikiangaliwa mara milioni 10 lakini hakuna mtu aliyeangalia au kuclick tangazo, huwezi kuingiza fedha yoyote.
Comments
Post a Comment