Skip to main content

Jinsi ya kuanzisha blog yako


Hapa ndio mahali husika katika kujifunza namna ya kuwa na blog yako na kuifanya iwe na mafanikio makubwa kama ambavyo wengine wamefanikiwa kupitia blog zao.

Kuna namna mbali mbali za kuwa na blog ila leo hapa nitazungumzia mbili tu ambazo ni rahisi sana. Kumbuka kuwa kuwa na blog yako mwenyewe hakuna gharama yoyote zaidi ya muda wako na ubunifu wako.
  1. BLOGGER Kupitia uwanja huo au platform hiyo inayomilikiwa na Google unaweza kuanzisha blog yako mwenyewe ambayo itabebwa na jina ulipendalo wewe mfano:- http://blogyako.blogspot.com, hapo ambapo nimekoleza kwa maandishi ya rangi nyekundu ndipo ambapo utaweka jina la blog yako. Utaratibu mzima utaupata wakati ukiwa unaisajiri blog yako Bofya hapa ili kutengeneza blog yako Create a new Blog 
  2. WORDPRESS Hapa pia utaratibu ni kama hapo mwanzo ila hizi ni nyanja (Platforms) tofauti na zinatofautiana vikolombwezo (features)  vya uboreshaji wa blogs. Hapa ukianzisha blog yako itabebwa na uwanja au platform ya wordpress. Namna ya jina la blog yako itakuwa katika mfano huu:- http://blogyako.wordpress.com. Ukitaka kuwa na blog kupitia wordpress tafadhali bofya hapa, Sign up For New Wordpress
Naamini hadi sasa umeisha elewa namna ya kuweza kuanzisha blog yako, wakati mwingine nitazungumzia jinsi ya kuweza kuwa na blog yako ikiwa na domain yako mwenyewe mf:- www.domainyako.com  kwa leo nisikuchoshe naishia hapa.

Kama una maswali au maoni tafadhali walisiliana nami kupitia masakafrances6@gmail.com
Au 0628533534 whatsapp

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kutengeneza Channel Youtube.

Karibu tena ndugu msomaji na mtembeleaji wa blog yako pendwa ya Tanzania    ambayo inakupatia elimu itakayokusaidia kucopi na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayotokea kila leo. Katika makala ya leo tutaenda kuzungumzia namna ya kufungua channel ya youtube maarufu kama online TV . Makala hii itakwenda kukupa ujuzi wa namna ambayo utaweza kufungua channel ya youtube wewe mwenyewe, channel ambayo utaweza kuweka video zako na watu wengine wakapata kuziona. MAHITAJI 1 : G mail account 2: Kifaa chako cha kielectoniki (kama computer) 3: Internet connection HATUA ZA KUFUATA 1:Fungua mtandao wa youtube kwenye search engine yako mfano opera mini, mozila firefox. kisha tafuta (search) www.youtube.com kama hivi:- 2:Kisha baada ya hapo itafunguka na utatakiwa kuanza kwa ku  sign in  kama inavyoonekana hapa chini:- 3:Kisha baada ya hapo chagua  g mail  account yako ambayo uta  sign in  nayo ka...

Utapata kwa siku 60000 kupitia blog!!!

Ndio inawezekana na kwa namna rahisi au kwa namna ngumu kutokana na jinsi ambavyo umejipanga katika blog yako na njia ambazo unazitumia kutengeneza hela kwa blogu.   Kuna njia nyingi sana za kutengeneza hela kwa kutumia blogu kwa uchache ni  Google Adsense, Kuuza vitu, Watu kulipia kuona blog yako, Matangazo  n.k Nimeaainisha kwa ufupi namna ya kupata hela ila endelea kutembelea blog hii kwani nitakuwa nikielezea moja baada ya lingine kwa undani zaidi. Lakini yote kwa ujumla yanategemea mambo makubwa ya yafuatayo. IDADI /Traffic  – Hapa idadi inayozungumziwa ni ya watu wanaotembelea blogu yako kwa siku. Kama blog yako ina watembelaaji wengi kwa siku kiasi cha kufikia 1000 basi ni wazi kuwa utakua katika nafasi nzuri ya kutengeza hela katika blog yako. Kwani IDADI/Traffic kubwa ya watembeleaje itavutia watangazaji katika kutangaza kwa blog yako. MADA /CONTENT  – Hapo jambo la kuzingatia ni kuwa blogu yako yajihusisha na nini zaidi...