Ndio inawezekana na kwa namna rahisi au kwa namna ngumu kutokana na jinsi ambavyo umejipanga katika blog yako na njia ambazo unazitumia kutengeneza hela kwa blogu.
Kuna njia nyingi sana za kutengeneza hela kwa kutumia blogu kwa uchache ni Google Adsense, Kuuza vitu, Watu kulipia kuona blog yako, Matangazo n.k Nimeaainisha kwa ufupi namna ya kupata hela ila endelea kutembelea blog hii kwani nitakuwa nikielezea moja baada ya lingine kwa undani zaidi.
Lakini yote kwa ujumla yanategemea mambo makubwa ya yafuatayo.
- IDADI /Traffic – Hapa idadi inayozungumziwa ni ya watu wanaotembelea blogu yako kwa siku. Kama blog yako ina watembelaaji wengi kwa siku kiasi cha kufikia 1000 basi ni wazi kuwa utakua katika nafasi nzuri ya kutengeza hela katika blog yako. Kwani IDADI/Traffic kubwa ya watembeleaje itavutia watangazaji katika kutangaza kwa blog yako.
- MADA /CONTENT – Hapo jambo la kuzingatia ni kuwa blogu yako yajihusisha na nini zaidi. Je ni habari, Mitindo? Mapishi? Urembo? Mauzo? . Na katika hilo swala unalojihusisha nalo uko makini kiasi gani ? Ni muhimu kuwa makini na kazi unayoifanya katika blogu na kuwa na habari au maelezo ya kutosha ili kuwavutia wasomaji wa blogu yako.
Hayo ni mambo makuu mawili ya kukuwezesha wewe kupata hela katika blog yako. Kwani watembeleaji zaidi inaleta watangazaji zaidi.
Nisikuchoshe kwa leo. Hadi wakati mwingine tena kwa maoni au maswali wasiliana nami kwa barua pepe masakafrances6@gmail.com
Comments
Post a Comment