Skip to main content

Jinsi ya Kutengenezs App za Android

Ulimwengu kwa sasa umekua sana kiasi kwamba karibia huduma zote unazipata kupitia simu yako ya mkononi, hii imesababisha watoa huduma wote ambao hutoa huduma mtandaoni kulazimika kutengeneza programu (App) kwaajili ya huduma zao, lakini katika kufanya hivyo bado unakutana na changamoto kwani ni lazima kuajiri watu kwaajili ya kufanya hivyo ndio mana leo Tanzania Tech tunakuletea njia hii ya kutengeneza app za android bila kuwa na ujuzi wowote maalum.
Kumbuka hauitaji ujuzi mkubwa kufanya hivi bali unaitajika kuwa na kompyuta yenye uwezo wa kuunganisha internet pamoja na logo na picha mbalimbali za kuweka kwenye programu yako. Ni vyema kuangalia kwanza matumizi kisha ndipo ujue jinsi ya kutengeneza picha na logo za kuweka kwenye App au programu yako, pia ni vizuri kuwa na simu ya android kwaajili ya kutest programu yako kabla ujaamua kuipost kwenye masoko ya Android kama Play Store au Amazoni Store.
Kwa kuanza ni vyema ukajua kuwa ili kutengeneza programu hii ni vyema ukajua unataka kutengeneza programu ya aina gani zifuatazo ni tovuti 10 zitakazo kuwezesha kutengeneza programu mbalimbali kutokana na maitaji yako, lakini sisi tutatumia tovuti ya Adromo kama mfano wetu wa leo.
  1. Mobile Roadie
  2. TheAppBuilder
  3. Appy Pie
  4. AppMachine
  5. BiznessApps
  6. BuzzTouch
  7. Good Barber
  8. Kinetise
  9. Andromo
  10. Como DIY
Kwa kuanza ingia kwenye tovuti ya Andromo kisha tengeneza akaunti kwenye tovuti hiyo, hakikisha unatumia email au barua pepe ambayo utaweza kuingia kwa muda wowote hii ni muhimu sana kwani programu yako itatumwa kwenye barua pepe hiyo baada ya kumaliza kutengeneza programu hiyo, hivyo hakikisha unatumia email sahihi.
Baada ya kujisajili na kuhakiki akaunti yako ingia kwenye akaunti yako kisha utaona mahali palipo andikwa Create New App bofya hapo kisha utaletewa sehemu ya kujaza jina la project hapo hakikisha una andika jina la programu yako kisha bofya Create, baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ulio andikwa Your App Activities hapo utatakiwa kuweka aina ya vitu ambavyo unataka programu yako ifanye, vitu vyote vinapatikana kwa kubofya sehemu iliyoandikwa Add an Activitiesifuatayo ni list ya vitu ambayo utatumia na kazi zake.
  • About – Hapa utaweka ukurasa wa kuhusu programu yako au wewe
  • Audio Player – Hapa utaweza kuweka sehemu ya kucheza muziki
  • Contact – Hapa utaweza kuweka anwani yako
  • Custom Page – Hapa utaweza kuweka ukurasa wowote unaotaka
  • Email – Hapa utaweza kuweka barua pepe
  • Facebook – Hapa utaweza kuweka ukurasa wa facebook
  • Flickr – Hapa utaweza kuonyesha picha kutoka mtandao wa Flick
  • Google Play – Hapa utawea kuonyesha link kwenda kwenye Google Play
  • HTML Archive – Hapa utaweza kuweka ukurasa unaotumia HTML
  • Map – Hapa utaweza kuweka ramani
  • PDF – Hapa utaweza kuweka file la PDF
  • Phone – Hapa utaweza kuweka namba ya simu
  • Photo Gallery – Hapa utaweza kuweka picha mbalimbali
  • Podcast – Hapa utaweza kuweka mfumo wa Podcast
  • RSS Feed – Hapa utaweza kuweka RSS fee ya blog yako
  • SHOUTcast Radio – Hapa utaweza kuweka radio kwenye app yako
  • Twitter – Hapa utaweka ukurasa wao wa Twitter
  • Website – Hapa utaweka tovuti yako
  • YouTube – Hapa utaweka ukurasa wako wa Youtube
Chagua aina ya kitu ambacho unataka programu yako ifanye kisha jaza vitu utakavyo ulizwa kisha endelea mbele kwa kuchagua sehemu ya Style hapo utaweza kuchagua rangi pamoja na aina ya style ambayo unataka programu yako iwe, baada ya hapo endelea mbele kwa kuchagua sehemu ya dashboard hapo utaweza kuchagua aina ya dashbord unayotaka kutumia kwenye app yako kisha save alafu endelea mbele kwa kuchagua Service tumeruka Monetize kwa sababu kwa hii ni app ya bure hivyo hutoweza kuweka matangazao mpaka hapo utakapo lipia kwenye tovuti hiyo kwa maelezo zaidi bofya hapa.
Tukirudi kwenye sehemu ya Serviceweka namba yako ya Google Analytics ili kujua watu wangapi wanaangalia vitu kwenye programu yako, kisha nenda hatua ya mwisho ambayo ni kutengeneza app yako, sehemu hii inapatikana kwenye Build chagua sehemu hiyo kisha chagua sehemu ya Build My App Hapo subiri kidogo baada ya muda kidogo utapokea barua pepe yenye link ya kudownload App au programu yako.
Ukimaliza hatua zote hizo utakuwa umamaliza kutengeneza programu yako ya kwanza ya Android bila hata kuwa na ujuzi wowote maalum, kama utakuwa unataka kufanya mabadiliko yoyote unaweza kuingia kwenye akaunti yako kisha fuata hatua hizo hapo juu kisha tengeneza tena app yako, kama kuna mahali umekwama usisite kutuandikia hapo chini kwenye maoni na tutakuelekeza.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kutengeneza Channel Youtube.

Karibu tena ndugu msomaji na mtembeleaji wa blog yako pendwa ya Tanzania    ambayo inakupatia elimu itakayokusaidia kucopi na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayotokea kila leo. Katika makala ya leo tutaenda kuzungumzia namna ya kufungua channel ya youtube maarufu kama online TV . Makala hii itakwenda kukupa ujuzi wa namna ambayo utaweza kufungua channel ya youtube wewe mwenyewe, channel ambayo utaweza kuweka video zako na watu wengine wakapata kuziona. MAHITAJI 1 : G mail account 2: Kifaa chako cha kielectoniki (kama computer) 3: Internet connection HATUA ZA KUFUATA 1:Fungua mtandao wa youtube kwenye search engine yako mfano opera mini, mozila firefox. kisha tafuta (search) www.youtube.com kama hivi:- 2:Kisha baada ya hapo itafunguka na utatakiwa kuanza kwa ku  sign in  kama inavyoonekana hapa chini:- 3:Kisha baada ya hapo chagua  g mail  account yako ambayo uta  sign in  nayo ka...

Jinsi ya kunufaika na blog au tovuti yako

Naam ni wengi sana wamekuwa wakianzisha blog au tovuti na kuishia njiani bila kuona mafanikio. Hapa nitazungumzia mambo makuu ambayo kama ukizingatia basi utafanikiwa katika blogu yako au tovuti. Kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kuanzisha blogu au tovuti yako. MADA /TOPIC   ni swala la muhimu sana kuzingatia kabla hujaanzisha blogu au tovuti yako. Wengi  wemeshindwa kutoka na kutokujipanga katika swala hili. Kama unataka kuwa na blog kwa ajili ya habari basi uwe umejipanga vizuri katika kupata habari mpya na sio kunakili kutoka katika blog zingine za habari. Wadau wengi wanaanzisha blogu ila hawaoni mafanikio kwa vile hawana kitu cha kuvuta wadau katika blogu zao. ·            8020fashions  ni moja ya blog ambayo imefanikiwa sana hapa Tanzania, mwanadada huyo yeye amejikita katika mambo ya wanawake. Hachanganyi mambo. ·            ...

Jinsi ya kuanzisha blog yako

Hapa ndio mahali husika katika kujifunza namna ya kuwa na blog yako na kuifanya iwe na mafanikio makubwa kama ambavyo wengine wamefanikiwa kupitia blog zao. Kuna namna mbali mbali za kuwa na blog ila leo hapa nitazungumzia mbili tu ambazo ni rahisi sana. Kumbuka kuwa kuwa na blog yako mwenyewe hakuna gharama yoyote zaidi ya muda wako na ubunifu wako. BLOGGER  Kupitia uwanja huo au platform hiyo inayomilikiwa na Google unaweza kuanzisha blog yako mwenyewe ambayo itabebwa na jina ulipendalo wewe mfano:- http:// blogyako .blogspot.com, hapo ambapo nimekoleza kwa maandishi ya rangi nyekundu ndipo ambapo utaweka jina la blog yako. Utaratibu mzima utaupata wakati ukiwa unaisajiri blog yako Bofya hapa ili kutengeneza blog yako  Create a new Blog   WORDPRESS  Hapa pia utaratibu ni kama hapo mwanzo ila hizi ni nyanja (Platforms) tofauti na zinatofautiana vikolombwezo (features)  vya uboreshaji wa blogs. Hapa ukianzisha blog yako itabebwa na uwanja au platform...