Wajasiriamali wengi wamekuwa wakitafuta mbinu mbalimbali za kufanya biashara aidha kwa kuuza huduma au bidhaa. Lakini wachache sana hasa Afrika ambao wanafikiria kufanya biashara katika intaneti. Kuna mbinu nyingi tofauti za kufanya biashara katika intaneti ambazo zinatoa fursa kwa wajasiriamali kujiongezea kipato. Kinachohitajika ni simu au kompyuta yenye kuunganishwa na mtandao wa intaneti na pia kuwa umejiunga na mitandao ya kijamii ,au mmiliki wa tovuti au blogu (ambazo unaweza kupata bure) au barua pepe. Zifuatazo ni baadhi ya programu zinazokuwezesha kupata fedha kupitia intaneti: 1. Kuuza Bidhaa za Biashara Yako Kupitia Tovuti Unaonesha biadhaa zako na bei,wanunuaji wanaziona na kuweka oda ya manunuzi. Wanalipa kwa Kadi ya Benki Credit /Debit Card) na fedha inaingia katika akaunti yako benki. Au kwa kutumia malipo kwa mfumo wa simu kama M-Pesa ,Tigo Pesa na Airtel Money kwa Tanzania. 2. Kuuza bidhaa za biashara ya watu wengine kupitia tovuti Unajisajili na baad...